Recent Comments

HAWA NI WACHEZAJI WENYE UMRI ZAIDI YA MIAKA 40 LAKINI BADO WANAENDELEA NA SOKA,YUKO ANAETAJWA KUWAFATA..

 Rivaldo – Kiungo wa zamani wa Barcelona, Ac Milan na timu ya taifa ya Brazil kwa
 sasa anaichezea timu ya Sao Caetano inayoshiriki ligi daraja la pili, alishawahi
 pia kucheza kwenye club ya Kabuscorp aliyoifungia magoli 11 kwenye mechi 21.
 David James – ni kipa wa zamani wa England na Liverpool na kwa sasa
 anaichezea Bournemouth ya ligi daraja la kwanza England akiwa na umri wa miaka 42.
 Mark Schwarzer ni kipa wa Australia anaeichezea Fulham, watu wengi
wanausahau umri wake wanapomuona uwanjani na hii
inatokana na wepesi wake golini.
 Paulo Maldini (44) – ni beki wa zamani wa AC Milan na timu ya Taifa ya Italia,
 alicheza mechi zaidi ya 900 akiwa na Milan na mechi 126 akiwa na timu ya taifa,
 amewahi kutwaa Mataji matano ya ligi ya mabingwa, saba ya Seria A na alistaafu
akiwa na umri wa miaka 41 na jezi yake namba 3 ikastaafishwa kwa heshima yake.
 Derek May ameripotiwa kuwa mchezaji mwenye umri mkubwa lakini anaecheza
 mpira kwa kiwango cha juu kabisa, umri wake ni miaka 74 ambapo amecheza kwenye
 mechi zaidi ya elfu mbili huku akifunga magoli zaidi ya 1300.
Kutokana na ukali alionao bado, mchezaji Didier Drogba ametajwa kwamba nafasi
yake kwenye list ya wachezaji walioendelea kucheza soka baada ya kufikisha
umri wa miaka 40 iko wazi, hiyo ni kutokana na ubora alionao sasa hivi japo umri
 wake ni miaka 34, anaingiza miaka 35 march 11 2013 siku tano zijazo.

Share on Google Plus

About Wasafi

    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments:

Post a Comment