VIDEO inayomuonesha msanii wa filamu Bongo, Shamsa Ford
akijifungua imezua kizaazaa baada ya mtu asiyejulikana
kuichukua bila ridhaa ya mhusika na kuisambaza kwa watu mbalimbali.
Akizungumzia suala hilo hivi karibuni, rafiki wa karibu
wa Shamsa alisema kuwa, video hiyo msanii huyo
alirekodiwa kwa ajili ya kumbukumbu zake lakini
ameshangaa kusikia kuna baadhi ya watu wanayo. “Yaani video hiyo imezua kizaazaa, Shamsa anahaha
kumjua aliyeisambaza lakini pia anahakikisha
haiwafikiii watu wengine na vyombo vya habari
kwani inamuonesha hatua kwa hatua akijifungua,”
kilisema chanzo hicho Baada ya kuzipata taarifa hizo, mwandishi wetu alimtafuta
Shamsa ambaye alisema:“Kiukweli nimeumia sana,
hiyo video ni kwa ajili ya kumbumbuku zangu,
kwa nini mtu aichukue na kuisambaza bila
ridhaa yangu? Imeniletea matatizo makubwa.”
|
0 comments:
Post a Comment