Recent Comments

MAELFU WAMIMINIKA KUMZIKA MAMA MZAZI WA BARNABA(BI MARIAMU ARUBETH)

''Salamu za pole na rambi rambi ziwafikie wafiwa wote but zaidi
 kwa msanii mwenzangu Barnaba Elias
kwa kupotelewa na mama yake mzazi siku ya Jumamosi ....
Pole sana ndugu sote ni wasafiri na duniani tupo kwenye
safari mbele yake nyuma yetu mwenyezi Mungu aipumzishe
 roho ya mama yetu Mariamu Arubeth mahala pema
peponi.AMINA''Nipo mbali kwa sasa,nipo comoro kweye tour
 lakini familia yangu
itajumuika nawe familia yenu kwa hali na mali
kwenye kipindi hiki
kigumu unachopitia kumpoteza mama yako mpenzi!!


Zifuatazo ni picha za Mazishi Ya Mama mzazi wa Barnaba kuanzia
nyumbani hadi makaburini....
Mama angu mzazi bi Sandrah ambae alienda kuniwakilisha akiwasili maeneo ya kigogo
msiba ulipokuwepo akiwa na
dada angu Esmah Khan....
Umati wa watu ukiwa umekusanyika nyumbani kwakina
Barnaba  kutoa heshima za mwisho..!
Familia wakitoa heshima za mwisho.....!!

Ni huzuni na sintoamini utawala kipindi hiki inapofika kuagana
 mara ya mwisho na mpendwa wako....
Barnaba akiagana na Mama ake kwa mara ya mwisho.....!!


Madee akiwa na  Lady Naa......!!

Joh Makini baada ya Kuaga Mwili.....!!
Baadhi ya wanakikundi wanaounda Tanzania House of Talent (T.H.T)


Mwili ukiwa umepakiwa tayari kabisa kuelekea makaburini
kwaajili ya maziko kumpumzisha
Mama....!!


Esmah Khan & Hawa ntarejea walikuwepo
kuwafariji wafiwa...

Hapa mwili ukiwa umewasili makaburini tayari kabisa kwa maziko...!

Jeneza likishushwa kaburini na wanafamilia....!!


Barnaba akitupa mchanga wa mwisho kwenye kaburi la marehemu mama yake

Barnaba akionekana kuishiwa na nguvu kabisa mpaka kufikia
hatua ya kutokuweza kusimama,
ilibidi asaidiwe...!!
Mume wa Bi Mariamu Arubeth akiweka mchanga kaburini...!!
Jeneza likiwa ndani ya kaburi tayari kwa kuanza kufukiwa na mchanga.....!
Hyper Man HK alikuwepo pembeni na mwanamuziki Shilole...!!
Producer Lamar  wa Fishacrab Studio alikuwepo pia...!
Hali ile ya uchungu na kulia sana ilipelekea Barnaba kukosa
nguvu na kuzimia kwa dakika kadhaa...


Baada ya kuzinduka akisaidiwa kuingia kwenye gari kuwaishwa
Hospital kutokana na kupoteza nguvu kabisa...!!

Simple the Boy alionekana kuwa mbele kwenye
 ratiba ya makaburini
 kuakikisha mipango inaenda sawa...!!


Mume wa Marehemu akisimika msalaba kaburini
..!!
Msemaji wa familia akisoma historia fupi ya
 marehemu Mariamu Arubeth...!!







Msemaji wa Familia akitoa maelekezo 
kwa waombolezaji mara
 baada ya kumaliza shuguli a maziko...!!
Umati wa waombolezaji wakitawanyika makaburini baada
ya shuguli ya mazishi kukamilika...!!
Nashukuru mama yangu mzazi na familia yangu kwa
 ujumla kwa kuniwakilisha vyema kwenye
 msiba wa mama mzazi wa mwanamziki mwenzangu,Barnaba,hapa 
ilikuwa ni baada ya mazishi wakielekea nyumbani

Share on Google Plus

About Wasafi

    Blogger Comment
    Facebook Comment

6 comments:

  1. Pole sana ndugu yangu.....Barnaba. Inatia uchungu sana kupotelewa na mpendwa mama mzazi. Lakini yote hayo mipango ya Jalali....wote tuko kwenye safari...

    ReplyDelete
  2. May her soul REST in ETERNAL PEACE.....

    ReplyDelete
  3. Pole sana ndugu yangu ni kweli inauma sana hata wala hatuna la kukusaidia ila mwenyenzi mungu akutie nguvu na akuondolee uchungu uliozidi ambao waweza kuleta madhara mengine.

    ReplyDelete
  4. pole sana barnaba napongezi zako platinum kwakuonyesha mshikamano kwa wenzako wanapofikwa namatatizo

    ReplyDelete
  5. Pole sana Barnaba, tuombe heri
    Mungu atakuongoza kusahau yote

    ReplyDelete
  6. pole sana barnaba mungu akutie nguvu na ailaze roho ya marehemu mahali pema peponi.inauma inasikitisha sana mungu akutie nguvu pole sana sisi wadau wa diamond tuko pamoja na wewe katika maombelezo

    ReplyDelete