Siku ya Jumatatu baada ya kuwasili Nairobi kutoka Mombasa usiku nilkikuwa na meeting na mwanangu aswa kabisa nadhani wamjua East Afrika nzima wanamjua huyu wakuitwa Mzazi Tuva wa kipindi kinachoonekana kupitia Citizen Tv cha Mambo Mseto.... Nia na madhumuni kama unavyoona tupo studio na mzazi tuva,hahhaaha sio kama mzazi Tuva anaimba laasha nguli huyu wa utangazaji nchini Kenya anasimamia baadhi ya wasanii chipukizi na katika kuombana ushauri wa kina zaidi aliniomba nitie maguu studio pale niweze kusikiliza ngoma mbili tatu za wasani wake ikiwemo kumsikiliza msanii wake ambae alikuwepo studio muda ule wa night kali.....
Baada ya kumsikiliza Msanii huyu chipukizi, anaejulikana nchini kenya kwa jina la Will Paul,Will ni msanii anaeimba muziki wa kumtukuza Mungu nikimaanisha Nyimbo za Injili lakini kiukweli ni kwamba aliniacha hoi pale nilipoona moja ya show alizofanya jukwaani uwa anaingia kwa nyimbo yangu ya Mawazo ,duh ebhanaa mshikaji kumbe mimi ndio role model wake,nilifurahi sana kuonana nae na niliona ni jambo la kheri kwake na kwangu kukutana pale.......
Baada ya muda kusikiliza Ngoma zake,Will alionesha kiu ya kutaka kufanya Ngoma na Mimi na Binafsi nilichoomba kwake ni yeye kuweza kufanya ngoma zaidi zenye uhalisia zaidi na kimaendeleo kadhaa kisha atampa msimamizi wa kazi zake ambae ni Mzazi Tuva anifikishie baada ya hapo ntakaa chini nijue ni nyimbo gani naweza mshika mkono chipukizi huyu mwenye kiu ya mafanikio,Dogo kiukweli anaimba lakini kama msanii mkubwa East Afrika na kati nazidi kumpa changamoto akazane na kazi za muziki na asikate tamaaa...
Muda ulivozidi kwenda si unajua tena ilikuwa midaa ya saa kumi alfajiri ilinipasa nihamshe nijongee hotelini mapema kseho niangalie utaratibu mwingine......
Big up n ni vizuri unafikiria kufanya kazi nae. Its true u can tell u r his role model just by listening to his songs an looking at his dressing code. Wote ni wako washike mkono.
Big up n ni vizuri unafikiria kufanya kazi nae. Its true u can tell u r his role model just by listening to his songs an looking at his dressing code. Wote ni wako washike mkono.
ReplyDelete