Mwanadada Rihanna azidi kuendelea kushamiri kwenye game ya muziki lakini amezidi kutengeneza vitega uchumi vingi vya kujiingizia hela zaidi ukiachia kazi zake za muziki..... Mwanamuziki huyo usiku wa tarehe 18 amezindua Manukato yake mapya kabisa ambayo yanaenda kwa jina la ROGUE ambayo Chupa ya kwanza ilinunuliwa kwa Dola za kimarekani elfu 52 kwenye Mnada na Tajiri kutoka nchini Thailand,jijini New York.... Manukato hayo ambayo yameanza kuuzwa kuanzia leo kwenye maduka wameonekana wakimiminika wakinadada kununua manukato hayo ambayo yanauzwa Dola 85 sawa sawa na laki moja na elfu kumi na moja elfu kwa pesa ya kitanzania...... Kwa wewe mdada na shabiki wa Rihanna unaweza pata manukato haya kwa kununua online na kupata manukato haya ambayo mwanamuziki huyu kwa mara ya tano sasa anatoa aina tofauti za manukato ya kike....
Hizi ni baadhi ya manukato na miaka zilivyotoka za Mwanadada Rihanna....
0 comments:
Post a Comment