Recent Comments

HUYU NDIE MSAJILI MPYA WA VYAMA VYA SIASA TANZANIA


Rais wa Jamhuri ya
 Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa 
Jakaya Mrisho Kikwete amemteua Mheshimiwa Jaji Francis S.K. Mutungi
 kuwa Msajili wa Vyama vya Siasa.
Taarifa iliyotolewa Dar Es Salaam 
leo, Jumatatu, Agosti 5, 2013, na kutiwa saini na Katibu Mkuu
 Kiongozi, Balozi Ombeni Sefue imesema kuwa uteuzi huo ulianza Ijumaa iliyopita Agosti 2, 2013.
Jaji Mutungi anachukua nafasi iliyoachwa
 wazi na aliyekuwa Msajili wa Vyama vya Siasa, Mhe. John Tendwa
 ambaye amestaafu Utumishi wa
 Umma kwa mujibu wa sheria.
Kabla ya uteuzi huo, Jaji Mutungi alikuwa Jaji wa Mahakama
 Kuu ya Tanzania, Kanda ya Dodoma.
Imetolewa na: 
Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais, 
Ikulu, DAR ES SALAAM.
Share on Google Plus

About Wasafi

    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments:

Post a Comment