Najua Blog yetu Imekuwa Kimya kwa muda wa siku mbili...... Lakini kutokana na Kazi za Kijamii ndo zilizochangia kukaa kimya kirefu...!! Nilikuwa Kigoma kwa Ziaraya Siku 2 Ambayo Mhe.Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,Jakaya Mrisho Kikwete, Alinialika Kujumuika nae kwenye Maadhimisho ya Miaka 36 ya chama cha Mapinduzi, Kitaifa yalifanyika Kigoma Mjini na Ufunguzi wa Uwanja wa Ndege wa Kigoma ...! Matatizo ya Mtandao pia yalichangia yakakwamisha uwezekanaji wa Habari kuwafikia kwa muda Muafaka.... Napenda kuwataharifu kuwa Nipo Dar Jijini.....na Kesho kuanzia Asubuhi Pitia Blog yako kama kawaida upate Matukio yote Muhimu yaliyojiri Mjini Kigoma... Show kali niliyopiga Nyumbani kwetu Mtoto wa Kimanyema..... Pia Pamoja na Kikao na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,Dr Jakaya Mrisho Kikwete Juu ya Unyonywaji wa Kazi za wasanii....!! Ni hayo tu kwa Sasa kwa Mengi zaidi Tukutane Kesho Hapa hapa panapo Majaaliwa...!! USIKU MWEMA....!!
0 comments:
Post a Comment