
Kila mtu katika maisha yake,kazi yake,masomo yake
na chochote anachokifanya huwa kuna watu/mtu
anaemvutia na kumpa changamoto
ya kufanya vizuri zaidi..binafsi kuna wanamziki wengi nyumbani na hata nje
mwanamziki ninaemkubali na kuliko mwanamziki yeyote duniani..amekuwa kioo
changu kila siku najitahidi
angalau niwe mwanamziki mzuri kama yeye na leo nataka nimuelezee kwa ufupi tu
alikoanzia kimziki mpaka sasa
Tunamfahamu kama Usher,lakini Serikali ya nchini mwake Marekani
wanamfahamu kama Usher Raymond IV ni marekani,alizaliwa october 14 mwaka 1978 ni mwimbaji,mwandishi wa nyimbo,dancer na mwigizaji ,anafanya R&B, soul, pop, hip hop, dance..
mwaka 1991 ndiyo umaalufu wa Usher ulianza baada ya kutoa
albamu yake ya pili iliyoitwa MY WAY,ambayo ndani yake wimbo
wa NICE&SLOW ulishika namba moja
kwenye Billboard hot 100,hakuishia hapo,albamu yake
iliyofata iliyoitwa 8701 ulitoa wimbo ambao wengi leo hii tumemfahamu
kupitia huo,unaitwa U REMIND ME ambao nao
ulishika namba moja kwenye Billboard hot 100
Mwaka 2004 alitoa albamu
iliyoitwa CONFESSIONS albamu iliyouza zaidi
ya nakala million 10 kwa marekani pekee na ilipewa
hadhi ya DIAMOND,ndani yake ilikuwa na vibao
vikali kama YEAH,BURN na MY BOO
na mwaka 2008 akatoa albamu ya HERE I STAND ndani
kukiwa na hit kali kama LOVE IN THIS CLUB ambao nao
ulishika namba moja kwenye Bllboard hot 100
March 30 mwaka 2010 Usher aliachia albamu
ya RAYMOND VS RAYMOND iliyoshika namba moja kwenye
US Billboard 200 chart na
albam hiyo ilipewa hadhi ya PLATNUMZ ndani yake
kukiwa na wimbo wa OMG wimbo ulioshika
namba moja kwenye Billboard na kumfanya
aweke rekodi ya mwanamziki aliyeshika namba moja
kwenye billboard kwa miongo mitatu
Usher alitangazwa kama moja ya best-selling artist kwa historia ya music
wa Marekani kwa kuuza zaidi ya copy million 23 kwa
Marekani pekee na mpaka sasa keshauza
zaidi ya copy million 65 Duniani na kumfanya
kuwa mmoja wa wanamziki wa miaka yote waliouza zaidi albamu zao .
kwa uchache tu huyu ndie Usher Raymond mwanamziki
anaeni inspire zaidi Duniani na najitahidi
kila siku nifikie mafanikio yake
kwani lolote lawezekana kwa yeyote mwenye nia na kujituma
Ndo ufanye Ucollaborate Nae coz Uwezo unao co unang'ang'ania ndani tu,expose Yourself Internationally Bro!!!
ReplyDeleteNimezaliwa siku moja na usher ndio kitu nilichofurahi.
ReplyDelete