Recent Comments

MFAHAMU KIUNDANI USHER RAYMOND,MWANAMZIKI ANAENI INSPIRE ZAIDI DUNIANI


Kila mtu katika maisha yake,kazi yake,masomo yake
 na chochote anachokifanya huwa kuna watu/mtu
 anaemvutia na kumpa changamoto 
ya kufanya vizuri zaidi..binafsi kuna wanamziki wengi nyumbani na hata nje 
ninaokubali kazi zao lakin Usher Raymond
he is the best,ndiye 
mwanamziki ninaemkubali na kuliko mwanamziki yeyote duniani..amekuwa kioo
 changu kila siku najitahidi
 angalau niwe mwanamziki mzuri kama yeye na leo nataka nimuelezee kwa ufupi tu
 alikoanzia kimziki mpaka sasa
Tunamfahamu kama Usher,lakini Serikali ya nchini mwake Marekani 
wanamfahamu kama Usher Raymond IV ni marekani,alizaliwa october 14 mwaka 1978 ni mwimbaji,mwandishi wa nyimbo,dancer na mwigizaji ,anafanya R&B, soul, pop, hip hop, dance..
mwaka 1991 ndiyo umaalufu wa Usher ulianza  baada ya kutoa
 albamu yake ya pili iliyoitwa MY WAY,ambayo ndani yake wimbo
 wa NICE&SLOW ulishika namba moja 
 kwenye Billboard hot 100,hakuishia hapo,albamu yake
 iliyofata iliyoitwa 8701 ulitoa wimbo ambao wengi leo hii tumemfahamu
 kupitia huo,unaitwa U REMIND ME ambao nao
 ulishika namba moja kwenye Billboard hot 100
Mwaka 2004 alitoa albamu
 iliyoitwa CONFESSIONS albamu iliyouza zaidi 
ya nakala million 10 kwa marekani pekee na ilipewa
 hadhi ya DIAMOND,ndani yake ilikuwa na vibao 
vikali kama YEAH,BURN na MY BOO
 na mwaka 2008 akatoa albamu ya HERE I STAND ndani
 kukiwa na hit kali kama LOVE IN THIS CLUB ambao nao
 ulishika namba moja kwenye Bllboard hot 100
March 30 mwaka 2010 Usher aliachia albamu
 ya RAYMOND VS RAYMOND iliyoshika namba moja kwenye
 US Billboard 200 chart na
 albam hiyo ilipewa hadhi ya PLATNUMZ ndani yake
 kukiwa na wimbo wa OMG wimbo ulioshika 
namba moja kwenye Billboard na kumfanya 
aweke rekodi ya mwanamziki aliyeshika namba moja
 kwenye billboard kwa miongo mitatu
Usher alitangazwa kama  moja ya best-selling artist kwa historia ya music
 wa Marekani kwa kuuza zaidi ya copy million 23 kwa 
Marekani pekee na mpaka sasa keshauza
 zaidi ya copy million 65 Duniani na kumfanya 
kuwa mmoja wa wanamziki wa miaka yote waliouza zaidi  albamu zao .
kwa uchache tu huyu ndie Usher Raymond mwanamziki 
anaeni inspire zaidi Duniani na najitahidi 
kila siku nifikie mafanikio yake 
kwani lolote lawezekana kwa yeyote mwenye nia na kujituma
Share on Google Plus

About Wasafi

    Blogger Comment
    Facebook Comment

2 comments:

  1. Ndo ufanye Ucollaborate Nae coz Uwezo unao co unang'ang'ania ndani tu,expose Yourself Internationally Bro!!!

    ReplyDelete
  2. Nimezaliwa siku moja na usher ndio kitu nilichofurahi.

    ReplyDelete