![]() |
Yobnesh Yusuph(Batuli) ambaye ni actress maarufu
Swahiliwood amemuomba Rais Jakaya Kikwete
kuliunda upya. Leo kupitia akaunti yake ya twitter
muigizaji huyo aliyejaaliwa mvuto na kupendwa na
mashabiki wengi wa filamu ali-tweet moja kwa moja
akimtaja JK kwa kuandika "ujumbe wa sikukuu ya
Eid kwako Mheshimiwa Rais wa Jamhuri ya Muungano
wa Tanzania, vunja baraza la BASATA uliunde upya".
Ingawa Batuli hakutaja moja kwa moja kwanini
baraza hilo linalosimamia sanaa ikiwemo tasnia ya
filamu nchini livunjwe lakini kwa muda mrefu
wasanii wakiwemo wa filamu na muziki wamekuwa
wakililalamikia baraza hilo kuwa linafanya mambo
kienyeji na baadhi ya wasanii kudai kukumbana na
urasimu wanapotaka kufanya kazi zao za sanaa.
Wengine wanadai hata hatua iliyopigwa sasa
katika sanaa nchini ni juhudi za wasanii wenyewe
pasipo sapoti ya kutosha kutoka BASATA. Baadhi ya
wasanii wa filamu wamekuwa pia wakitaka TAFF
ndiyo ipewe mamlaka kamili ya kusimamia shughuli
zote za tasnia ya filamu nchini kutokana na BASATA
kuwepo muda mrefu lakini Sanaa ya Tanzania bado
haijapewa hadhi ya sekta rasmi na kuwa na sera ya
kueleweka katika kumkomboa msanii na kuzidi kupiga hatua.
Hivi karibuni pia mwanamuziki Diamond Platinumz
alikaririwa akisema BASATA ndiyo wa kulaumiwa kwa
kutokuwa na tuzo nyingine za muziki mpaka sasa
kwakuwa chombo hicho kimekuwa kikiweka kauzibe
kwa watu wanaotaka kuazisha tuzo mbalimbali za
sanaa ikiwemo hata katika tasnia ya filamu.
Kama wewe ni shabiki wa Batuli basi m-follow
hapa BATULI-ACTRESS katika mtandao wa
twitter ili kupata updates zake
|
- Blogger Comment
- Facebook Comment
Subscribe to:
Post Comments
(
Atom
)

0 comments:
Post a Comment