MWANA MUZIKI mkongwe wa bendi ya muziki ya Msondo Ngoma Maalim Muhidini Gurumo ametangaza rasmi kuachana na kazi ya muziki baada ya kutoa albamu ya 60 tangu aanze kuimba nyimbo hapa nchini.
Akizungumza mbele ya waandishi wa habari jijijini Dar es Salaam hapo jana, Gurumo amesema kuwa kutokana na kuifanya kazi ya muziki kwa miaka 53, ameamua kustaafu na kuwaachia vijana waendelee na kazi hiyo.
Amesema kuwa kwa muda mrefu alikuwa nje ya familia yake kutokana na kurudi usiku wa manane hivyo kitendo cha kustaafu muziki kitamsaidia kwa asilimia kubwa kuwa karibu na familia yake
0 comments:
Post a Comment