Wakati tume ya kuchunguza matokeo mabaya ya kidato cha nne
mwaka 2012 ikiendelea na kazi, imebainika kuwa wanafunzi
waliokata rufaa kutaka mitihani yao isahihishwe upya wamefeli
zaidi baada ya
kusahihishiwa.Kwa mujibu wa taarifa kutoka ndani ya Baraza la
Mitihani la Taifa (NECTA) na Wizara ya Elimu na Mafunzo ya
Ufundi ambazo zimethibitishwa na baadhi ya maofisa, wanafunzi
waliokata rufaa wamefeli zaidi na hata walioongezewa alama
matokeo hayakubadilisha madaraja waliyopata awali.Habari
zinaeleza kuwa, wanafunzi waliokata rufaa NECTA kutaka
mitihani yao isahihishwe upya ni takribani 10,000 na kwamba
baraza bado limetoa muda zaidi kwa wengine wanaotaka kukata rufaa.
Vyanzo vya habari kutoka ndani ya NECTA viliieleza NIPASHE kuwa
mitihani kwa wanafunzi waliokata rufaa ilianza kusahihishwa
Machi 12 na kuhitimishwa Machi 15, mwaka huu na kwamba
wengi wamefeli zaidi.“Baada ya wanafunzi kadhaa kukata rufaa,
NECTA iliamua kuwaita walimu waandamizi katika masomo
yote na kuanza kufanya kazi ya kusahihisha mitihani hiyo upya
kwa umakini, kilichowashangaza walimu hao ni kuona kiwango
cha kufeli kimeongezeka,” alisema ofisa mmoja wa NECTA ambaye
aliomba jina lake lisiandikwe gazetini kwa maelezo kuwa siyo
msemaji wa baraza hilo.
Baadhi ya walimu walisema walioshiriki kusahihisha mitihani hiyo
walisema kuwa maoni yaliyokuwa yanatolewa na baadhi ya
watu kwamba matokeo mabaya ya mtihani huo yalitokana na
uchakachuaji, hayakuwa ya kweli.Katibu Mtendaji wa NECTA,
Dk. Joyce Ndalichako, akizungumza na NIPASHE jana alithibitisha kuwa
mitihani ya wanafunzi waliokata rufaa ilianza kusahihishwa Machi
12 mwaka huu.
Dk Ndalichako alisema hata hivyo, hana taarifa kama matokeo ya
wanafunzi hao yanaonyesha kuwa wanafunzi wengi wamefeli zaidi
kwa kuwa alikuwa safarini kikazi.“Unavyozungumza na mimi nipo
Arusha na wageni, sifahamu kama baada ya kusahihishwa upya
mtihani wa wanafunzi waliokata rufaa matokeo yamekuwaje, nitafahamu
baada ya kurejea Dar es Salaam Jumatano wiki hii,” alisema
Dk Ndalichako ambaye hata hivyo, hakutaja idadi ya wanafunzi
waliokata rufani.Dk Ndalichako alisema suala la kufeli zaidi wanafunzi
waliokata rufaa linawezekana kutokea kwa sababu kila mwaka
imekuwa ikijitokeza hali kama hiyo, hivyo ni jambo la kawaida.
Habari kwa Hisani ya Wizara ya Elimu Tanzania...
|
0 comments:
Post a Comment