The best Rapper kutoka kampuni ya weusi A’town Tanzania Nikki wa pili amefunguka kuelezea mistari aliyoandika kwenye single yake mpya nje ya kumi na nane (18) pamoja na mafanikio aliyoyapata baada ya kuuza DVD ya kubumkubam. Kupitia One2One Interview iliyokuwa hosted na Dulla Ambua kwenye kipindi cha Planet Bongo Eat Africa Tv jana usiku Nikki wa Pili alisema kwamba wakati alipo compose wimbo ya nje ya Boksi lengo lake ilikuwa ni kuandika mapenzi katika uhalisia sio nadharia. Mkali huyo alisema kuwa katika kipindi cha mwezi mmoja mafanikio aliyopata kwenye mauzo ya DVD ya Kubumkubam kupitia mtandao akishirikiana na kampuni ya fichuka ni nakala 745.
Akiwa kama msanii na msemaji wa kampuni ya weusi Rapper huyo alisema kuwa wiki ijayo itatoka video ya Joh Makini inayoitwa kiutu uzima na weekend hii G Nako ata Shoot video ya Mama Yeyoo huku Lord Eyes nae akisubiri kupokea kichupa cha single yake ya Baba la baba feat Ben Pol ambayo ameshoot na wa Denmark.
0 comments:
Post a Comment