Lionel Messi,Mchezaji kutoka Argentina na babake, Jorg
e wanatuhumiwa kuibia serikali ya nchi hiyo, kwa
kujaza fomu zizizokuwa za ukweli za marejesho ya
kodi kati ya mwaka wa 2007 na 2009.
Hata hivyo mechezaji huyo mwenye umri wa miaka
ishirini na mitano hajasema lolote kuhusiana na madai hayo.
Messi hulipwa Euro milioni kumi na sita kila
mwaka na ndiye mchezaji anayelipwa kiasi cha juu zaidi duniani.
Lakini mwendesha mashtaka Raquel Amado, aliwasilisha
nyaraka za mahakama nyumbani kwake kwa
mchezaji huyo katika mtaa wa kifahari wa Gava mjini Barcelona.
Jaji mjini humo ni sharti waidhinisha malalamishi
dhidi ya mshukiwa yeyote kabla hajafunguliwa mashtaka.
Messi na babake wanashukiwa kutumia kampuni
katika mataifa ya ngambo, mjini Belize na Uruguay
kuuza haki za kutumia picha ya mchezaji huyo.
Mchezaji huyo na babake wanatuhumiwa
kutumia kampuni hizo zilizoko nje ya Uhispania,
ambako anaishi na kucheza soka ya kulipwa, kukwepa
kulipa kodi inayokisiwa kuwa pauni milioni tatu na nusu.
0 comments:
Post a Comment