Recent Comments

SHINDANO LA BONGO STAR SEARCH LIMERUDI TENA

Shindano la kusaka vipaji vya uimbaji muziki la Epiq
 Bongo Star Search, EBSS, leo limezinduliwa rasmi jijini Dar es Salaam.
 Uzinduzi huo uliofanyika makao makuu ya Zantel umehudhuriwa na
 Mkurugenzi wa Benchmark Production, Rita Paulsen a.k.a Madam
Rita ambaye ni mwanzilishi na mmoja wa majaji shindano hilo, Afisa
Biashara Mkuu wa Zantel, Sajid Khan pamoja mshindi wa shindano
hilo mwaka jana, Walter Chilambo.
 

Mwaka huu, EBSS ambayo itajulikana kwa kauli mbiu ya
 ‘KAMUA’ itaenda kufanya usaili kwenye mikoa sita ya Mbeya,
 Arusha, Zanzibar, Mwanza, Dodoma na Dar es Salaam.

Usaili utaanzia Dodoma tarehe 29 and 30 ya mwezi huu katika
 ukumbi wa Maisha Club, ikifuatiwa na Zanzibar tarehe 5 na 6
mwezi wa saba katika hoteli ya Bwawani. Mbeya usaili utakuwa
tarehe 10 hadi 11 mwezi wa saba pale club Vybes, Mwanza tarehe
14 hadi15 mwezi wa saba Club Fussion, na Arusha itakuwa
tarehe 20 hadi 21 mwezi wa saba Club Tripple A ikimalizikia na
 Dar es Salaam tarehe 26 hadi 28 pale Uwanja wa Taifa.


Share on Google Plus

About Wasafi

    Blogger Comment
    Facebook Comment

1 comments:

  1. KINACHOFANYIKA KATIKA BSS NI ISHARA YA KWAMBA MNAWAJALI VIJANA MBARIKIWE.NAOMBA PIA IANDALIWE NAMNA YA KUANDA BSS FOR HANDICAP PEOPLE MAANA KUNA WALEMOVU WENGI WENYE VIPAJI AMBAO HAWAFIKISHWE KWENYE ENEO LA TUKIO AMBAO NAO WANAHITAJI FURSA HIZO PENGINE TUNAWAPONGEZA MAANA VIJANA WENGI SANA WAMEJIPATIA KIPATO IKIWA NI PAMOJA NA KUJIAMINI KWAMBA WANAWEZA

    ReplyDelete