Mwanamuziki Chris Brown amepandishwa kizimbani kwa saa kisha kuachiwa kwa dhamana kutokana na msala wa kugonga na kukimbia unaomkabili alioupata miezi kadhaa iliyopita... Katikati ya wikii hii,jamaa alijisalimisha mwenyewe katika kituo cha polisi Van Nuys kabla ya kupandishwa mahakamani kujibu mashitaka yanayomkabili alikana. ''Haikuwa kugonga na kukimbia kama nilivyoshitakiwa,hakuna mtu wala gari lililoumia siku ya tukio,''Alikanusha Chris Mwanamuziki huyo aliachiwa kwa dhamana hadi kesi hiyo itakapotajwa tena ambapo amewaomba mashabiki zake wasiwe na wasiwasi na wajiandae kupokea album yake mpya ya X august 20 mwaka huu...
0 comments:
Post a Comment