ZUWENA MOHAMED ‘SHILOLE’Alianzia kwenye filamu kisha akajiingiza kwenye muziki. Kwa mujibu wake mwenyewe, aliwahi kukiri kuwa aliingia kwenye fani hizo kwa ajili ya kujitafutia kipato ili kulea wanaye. Aliolewa ndoa ya kwanza huko kwao Tabora na kuzalishwa mtoto mmoja kisha ndoa ikaota mbawa. Hakukaa muda mrefu akapata mwanaume mwingine ambaye alimpa ujauzito na kuzaa mtoto wa pili. Aliwahi kusema kati ya wanaume hao, hakuna anayemsaidia kulea.
MIRIAM JOLWA ‘JINI KABULA’Alianzia kwenye uigizaji kisha urembo na sasa ameongezea muziki. Amezaa na Mkurugenzi wa Tuesday Entertainment, Tuesday Kihangala ‘Mr Chuz’ ambapo walijaliwa kupata mtoto mmoja wa kike na baada ya hapo mapenzi yakaisha. Kwa kuwa mapenzi yalikwisha, Jini Kabula alibaki na mwanaye akimlea mwenyewe japo Mr Chuz huwa anampiga ‘tafu’.
SNURA MUSHI Alianzia kwenye uigizaji kabla ya hivi karibuni kujikita pia katika tasnia ya filamu. Ana mtoto mmoja wa kike. Anakiri kuwa tangu akiwa mjamzito baba mtoto wake aliingia mitini. Mpaka sasa anamlea mwanaye mwenyewe kupitia sanaa ya filamu na muziki.
MAUNDA ZORROAlipata umaarufu kupitia muziki na baadaye akaongezea uigizaji. Ana mtoto mmoja na huwa hapendi kumwanika mwanaume aliyemzalisha ambapo mpaka sasa anaishi nyumbani kwa baba yake, mzee Zahir Zorro na hakuna dalili zozote za ndoa.
0 comments:
Post a Comment