Ile tume iliyoteuliwa na Waziri Mkuu Mizengo Pinda february 22 2013 kuchunguzamatokeo mabaya ya mitihani ya kidato cha nne 2012 tayari imeanza kazi yake ambayo uharaka wa kupata matokeo ya utatokana na ushirikiano kutoka kwa wadau wa elimu kwenye mikoa mbalimbali itakayochunguzwa.
Mwenyekiti wa hiyo tume ambae ni Profesa Sifune Mchone amesema kwa kuanzia, wameanza kufanya uchunguzi Dar es salaam, mkoa ambao matokeo yalikua mabaya tofauti na miaka iliyopita ambapo kwa ujumla nchi nzima zaidi ya asilimia 60 ya Wanafunzi walifeli kwa kupata daraja la mwisho.
0 comments:
Post a Comment